Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Vyanzo mbalimbali vya kimataifa vilieleza kuwa hatua za Iran zilithibitisha uwezo wake wa kujilinda, kulinda heshima ya Umma wa Kiislamu, na kusimama kidete dhidi ya uonevu wa Marekani na Israel. Wachambuzi wengi wa siasa za kimataifa walikiri kuwa uongozi wa Sayyid Khamenei umeifanya Iran kuwa mhimili wa upinzani dhidi ya ubeberu wa dunia.
Katika mitandao ya kijamii na majukwaa ya kisiasa, kauli moja ilijitokeza kwa nguvu ikisema:
“Huyu ndiye binadamu mwenye nguvu kubwa kuliko wote kwa sasa duniani.”
Kauli hiyo ilielekezwa kwa Sayyid Khamenei, kiongozi ambaye kwa miaka mingi ameiongoza Iran bila kuyumbishwa na vitisho, vikwazo wala mashinikizo ya kimataifa.

MSIMAMO WA IRAN
Iran imeendelea kusisitiza kuwa msimamo wake si wa uchokozi bali ni wa kujilinda, kulinda haki za mataifa yaliodhulumiwa, na kupinga sera za kibabe zinazokanyaga heshima ya mataifa huru.
ATHARI KIMATAIFA
Hatua za Iran zimeongeza heshima yake miongoni mwa mataifa huru na harakati za ukombozi, huku zikiwapa matumaini watu wanaopinga ubeberu, dhulma na unyonyaji wa kimataifa.
Kwa uongozi wake wa busara na ujasiri, Ayatollah Sayyid Ali Khamenei ameonesha kuwa Iran si taifa la kuamrishwa, bali ni dola huru inayojitambua, inayolinda hadhi yake, na inayosimama upande wa haki.
Hongereni sana kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran - ipo siku dunia itawaelewa tu.
Your Comment